编辑: gracecats 2016-09-04

102 Hali au jiha mbalimbali za nafsi moja

103 Nafsi mbalimbali zikishirikiana katika umilele . . . .

104 Nafsi mbalimbali zenye sifa tofauti kabisa.108 Nafsi tofauti zenye sifa zifananazo zilizo sawa . . . .

113 7. MAGEUZI YENYE KUENDELEA YA UKRISTO

116 Wafuasi wa kwanza wa Yesu

116 Kazi ya Mtakatifu Paulo

119 Uhakika wa Yesu

120 Kuendelea Dini

123 Upeo wa mwisho wa maendeleo ya dini

124 8. UKRISTO KATIKA ZAMA HIZI

127 Ukristo na ukoloni.127 Ujaji wa Yesu Kristo mara ya pili

131 Masihi Aliyeahidiwa.137 Mwisho

144 NYONGEZA I

149 NYINGEZA II.151 vi UTANGULIZI Dhati ya Yesu ni ya muhimu sana kwa ulimwengu wa kisasa. Umuhimu wake haukomei ulimwengu wa Kikristo pekee, bali unaenea hadi kwa dini nyingi pia mashuhuri kama vile dini ya Kiyahudi na Islam. Kama dini hizo zenye nguvu zikielewana kuhusu uhakika wa dhati ya Yesu, ujaji wake wa mara ya kwanza na ule wa mara ya pili, hapo bila shaka uelewano huo utatatua matatizo mengi yanayowakabili wanadamu katika zama hizi. Kwa bahati mbaya mambo ya msingi ya maisha ya Yesu, shabaha yake, nadharia na dhati yake vimeeleweka visivyo kabisa. Katika kufahamu mambo hayo, dini hizo zinazozana vikali sana zenyewe kwa zenyewe hata kwamba ushindani mkali unazuka baina yao. Tunapochunguza hakika ya tukio la msalaba na kutafakari yale yaliyotukia na kwa nini yalitukia na pia katika wokovu na hekima yake, tunapata maelezo yanayopinzana kutoka njia tofauti za zamani. Nimechagua kutumia mantiki pekee kwa kuzungumzia swala hilo. Naamini ya kwamba hilo ndilo jukwaa lililo sawa kwa wote linaloweza kutumiwa kwa maongezi yafaayo. La sivyo, majadiliano yoyote juu ya msingi wa maandiko pamoja na maelezo ya aina tofauti yataelekeza kwenye mgogoro wa mabishano ambao kutoka nje yake kutakuwa vigumu. Miaka elfu mbili imekwisha pita, hata hivyo kwa msingi wa maandiko peke yake hakuna suluhisho ambalo litakubaliwa na wote lililokwisha fikiwa hadi sasa. Kiini cha tatizo ni tegemeo la baadhi ya maandiko ambayo yanapinzana yenyewe kwa yenyewe. Pia matatizo makubwa yamejitokeza kwa kukua polepole kutokana na kutoelewana kulikoizunguka historia ya Yesu Kristo. Mtazamo wa picha ya kihistoria kama kawaida huelekea kutiwa

1 ukungu na hufifia. Kwa vyovyote muda wa miaka elfu mbili kupita si kikwazo cha kawaida kwa kufahamu matukio yaliyotukia zama za uhai wa Yesu. Mantiki ya binadamu na akili yake zikisaidiwa na mwanga wa ujuzi wa elimu ya sayansi hazitegemei imani ama rangi au dini ya mtu. Bali ziko sawa kwa watu wote na dini zote. Ni mantiki peke yake inayoweza kutupatia msingi kwa kuleta umoja wa fikra. Nitajaribu kutathmini tatizo hili kwa njia mbalimbali. Hebu nianze kwa kuuchunguza Ukristo jinsi wanavyoufahamu Wakristo wenyewe na kisha kuuchanganua kwa kuuangalia na hadubini ya kiakili na hoja. Lakini sina budi kusisitiza ya kwamba simaanishi kwa vyovyote kutokuwa na heshima kwa Wakristo ama Yesu Kristo. Nikiwa Mwislam ni nguzo ya imani yangu kumwamini Yesu Kristo na kumkubali kwamba yu Nabii wa Mungu mwenye shani na utukufu, aliyekuwa na daraja la pekee baina ya Manabii wa Kiisraeli. Lakini pale ukweli unapoamuru kwa haki na busara, akili na fahamu ya binadamu, mtu hawezi kujizuia kusahihisha fikra zake kuhusu Ukristo. Sina shabaha ya kuleta mfarakano baina ya Wakristo na Kristo, bali napenda kuwasaidia Wakristo kusogelea karibu zaidi uhakika kumhusu Yesu Kristo na kujitenga mbali na hadithi zilizobuniwa kumhusu yeye. Zama zinaweza kupotoa hakika na kuigeuza kuwa hadithi na ngano zisizo za kweli. Athari ya hadithi hizo za kubuniwa humpeleka mtu mbali na hakika halisi za maisha. Matokeo yake ni kwamba imani inakuwa mawazo ya kubuni tu, yasiyo ya kweli, yasiyo sawa. Ambapo imani ya kweli inayo asili yake katika mambo na matukio ya kweli ya kihistoria, ni ya hakika halisi na ina nguvu ya kutosha kuleta mabadiliko katika jamii ya binadamu. katika jitihada ya kufahamu imani ya kweli na mafunzo hasa ya Yesu, ni jambo la muhimu kabisa kuchuja uhakika kutoka na ngano za kubuniwa. Kutafuta ukweli ndiyo shabaha hasa ya zoezi hili lote. Natumai mtaniwia radhi na kufahamu kwamba simaanishi kudharau imani ya mtu ama kuchochea hisia zake.

下载(注:源文件不在本站服务器,都将跳转到源网站下载)
备用下载
发帖评论
相关话题
发布一个新话题